NJIA ZA UPANDAJI MITI
Kuna njia mbali mbali za upandaji miti duniani ambazo zinaifanya mimemea iweze kukuwa kwa haraka sana bila ya kumwagilia mbolea yoyote.kama video inavyoonesha hapa chini.katika upandaji wetu wa miti unakuwa kwa kiwango kikubwa unakuwa hauna ujuzi na taaluma mzuri ndo maana watu wengi wanakuwa hawazalishi mimea mingi sana katika eneo kubwa sana.
upandaji wa mimea
Unaweza kulima kabichi msimu wote wa mwaka. Soko lake ni la uhakika katika kipindi chote na ni muhimu kwa afya. Pia, linaweza kutumika kama malisho ya mifugo
Kabichi ni moja ya mazao yaliyomo katika jamii ya mimea inayojumuisha mimea ya kaulifulawa (cauliflower ), kabichi ya kichina na kale. Kwa kawaida kabichi hupandwa kwa msimu mmoja, lakini iwapo itakuzwa kwa ajili ya kutoa mbegu hukuzwa zaidi ya msimu mmoja. Endapo inalimwa sehemu yenye maji ya kutosha, inaweza kulimwa msimu wote wa mwaka. Kichwa cha kabichi kinapofunga vizuri, hutumika kama chakula na huvunwa baada ya kufunga na kukomaa vizuri.
Mizizi: Mizizi ya kabichi hutawanyika ardhini vizuri. Kwa kawaida, huenda chini kiasi cha sentimita ishirini (20 sm), na hujitawanya kwa kiasi cha sentimita sabini na tano (75sm).
Shina: Shina la mmea wa kabichi huwa na rangi ya kijani au zambarau. Hii hutegemeana na aina ya kabichi, na kwa kawaida ni fupi.
Hali ya hewa: Kabichi hustawi vyema katika sehemu yenye hali ya baridi, hali ya joto jingi haifai kwa kabichi kwa kuwa huathiri uotaji na ukuaji wake. Joto jingi pia husababisha kulegea kwa vichwa vilivyofunga. Zao hili hustawi vema katika maeneo yenye mwinuko wa zaidi ya mita 100 toka usawa wa bahari.
Udongo: Zao hili linaweza kustawishwa kwenye udongo wa aina yoyote mradi tu udongo huo usiwe na chumvichumvi nyingi na usiotuhamisha maji. Udongo wa kichanga na ule usio na rutuba ya kutosha husababisha kabichi kukomaa upesi na kuzaa kabichi hafifu zenye vichwa vidogo.
Kitalu: Kitalu ni muhimu katika uzalishji wa zao hili. Ni vema kutengeneza matuta yenye upana wa mita moja, na urefu wowote kulingana na matakwa ya mkulima.
Mbolea za samadi na zenye asili ya chokaa zichanganywe vizuri kwenye udongo. Kiasi cha gramu 500 za mbegu huhitajika kwa hekta moja. Katika upandaji kwenye kitalu ni vizuri kutengeneza mistari katika tuta, umbali toka mstari hadi mstari uwe sentimita ishirini (20). Udongo kiasi kidogo utumike katika kufunika mbegu.
Baada ya mbegu kuota ni vizuri kupunguza baadhi ya miche na uwe katika kipimo cha sentimita 2-3 toka mche hadi mche.
Hii itasaidia kuwa na miche mifupi na yenye nguvu. Inafaa kunyeshea kitalu mara moja au mbili kwa siku na katika sehemu za joto ni vizuri kuweka kivuli katika matuta. Katika wiki ya tatu, hadi wiki ya nne, ni vyema kuondoa kivuli kidogo kidogo huku ukipunguza unyeshaji. Hali hii itasaidia miche isipate mshtuko wa uhamishaji shambani.
Kuhamisha na kupanda
Hamisha na kupandikiza miche shambani ikiwa na umri wa wiki nne, wakati huo miche ikiwa na majani manne ya mwanzoni na urefu wa kiasi cha sentimita kumi na mbili (12). Wakati wa upandaji, ni vizuri udongo ukashindiliwa kwenye kila mche. Inafaa upandaji ufanyike mara moja, na ni vizuri ukafanyika nyakati za jioni au asubuhi sana, na udongo uwe na unyevu wakati wote.
Nafasi kati ya mmea
Katika mstari hadi mstari inatakiwa iwe sentimita 60-75. Kutoka mmea hadi mmea ni sentimita 30-60. Pia sentimita 75-90 inaweza kutumika kati ya mstari na mstari.
Mbolea: Ni vizuri kuweka kiasi cha viganja 2-3 vya mbolea ya samadi iliyooza vizuri katika kila shimo.
Palizi: Wakati wa palizi ni vizuri mkulima akawa mwangalifu ili asiharibu mizizi. Wakati kabichi inapoanza kufunga hufunika ardhi, hivyo, husaidia kuzuia magugu yasiote, kwa wakati huu hakuna haja ya kupalilia.
Kuvuna: Kabichi hukomaa katika kipindi cha siku 60-100 tangu kupandwa. Kwa ajili ya kuuza ni vizuri kuvuna wakati vichwa vinapofunga vizuri na huwa na uzito wa kutosha kabichi iangaliwe na kutunzwa baada ya kuvunwa ili isikwaruzwe na kuoza kabla ya kutumiwa. Kwa kawaida hekta moja hutoa mavuno kiasi cha tani 50-80.
Aina za kabichi
Kuna aina nyingi za kabichi na zifuatazo ni miongoni mwa aina hizo:
Early Jersey wakefield – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5
Sugar loaf – Aina hii hukomaa mapema sana, kiasi cha miezi 2.5
Glory of enkhuizen – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5
Prize drumhead – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5
VIDEO YA UPANDAJI
VIDEO HII INAONYESHA JINSI YA UPANDAJI WA WA MAKEBICHI

Kilimo cha Kabichi
Muungwana Blog Thursday, March 09, 2017 Kilimo katika kuwatika mimea kuna namna mbalimbali ya uendeshaji au uzalishaji wa mazao vizuri au kwa kiwango cha juu.
Prize drumhead – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi
MBEGU YA MAHINDKANUNI 5 MUHIMU ZA KUFANYA KILIMO BORA CHA MAHINDI
KANUNI 5 MUHIMU ZA KUFANYA KILIMO BORA CHA MAHINDI : Moja kati mbinu ambazo zitakufanya uweze kulima kilimo chenye tija kujua kanuni ambazo zitakuzaidia kuweza kulima kilimo hicho, na kanunia hizo nitazieleze katika Makala haya. Mahindi ni zao muhimu linalo limwa katika maeneo ya kitropiki. Pia zao hili hulimwa katika udongo wenye uchachu pH 6-6.5. lakini pia hustawi zaidi kwenye maeneo yenye mwinuko wa 2500.
KANUNI YA KWANZA; Kutayarisha shamba mapema.
- Tayarisha shamba la mahindi mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu uliopita.
- Mahindi hustawi sehemu yenye udongo wenye rutuba na usiosimamisha maji.
- Moto usitumike wakati wa kuandaa shamba.
Faida ya kuandaa shamba mapema
- Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi kwa kutumia jembe lolote.
- Masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.
- Hupunguza magugu.
- Hupunguza wadudu waharibifu.
KANUNI YA PILI ; kujua wakati wa kupanda mbegu sahambani.
Wakati wa kupanda hutatanisha kwani mvua haitabiriki, Kama mvua hunyesha nyakati na majira yale yale ya mwaka basi kalenda ifuatayo inaonyesha tahere za kupanda zao la mahindi katika eneo lako.
- Mbeya na maeneo ya jirani, mwanzoni mwa mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni.
- Morogoro na maeneo ya jirani, Mwezi Januari katikati hadi Februari katikati
- Iringa na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni
- Songea na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Januari mwanzoni.
Kupanda mahindi mapema ni muhimu kwani uwezekano wa kuvuna mazao mengi ni mkubwa. Kwa mashamba makubwa makubwa sana wakati wa kupanda uwe wiki moja kabla ya mvua kuanza kunyesha na isizidi wiki mbili kabla ya mvua.
Isiwe mapema zaidi kwani mbegu zitaharibiwa na joto kati ya udongoni wadudu, panya, ndege na wanyama wengineo.
FAIDA ZA KUPANDA MAPEMA
- Mahindi yanapata mvua ya kutosha hadi kukomaa.
- Magonjwa kama yale ya ya majani (streak ugonjwa wa milia) hayatatokea au yatakuwa kidogo.
- c) Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na mahindi yastawi vizuri.
KANUNI YA TATU KUCHAGUA MBEGU BORA
Mbegu bora ni zile zilizo zalishwa kitaalamu.
- a) Ni safi hazijabunguliwa na wadudu.
- b) Huzaa mazao mengi.
- c) Hustahimili magonjwa.
AINA ZA MBEGU
- Mbegu aina ya chotara (hybrid)
- Aina ya ndugu moja (synthetic)
- Mbegu aina ya composite
Mbegu za kisasa zikitumiwa vizuri katika vizuri katika misingi ya kilimo zina uwezo wa kuzaa magunia 50-80 au tani 5.5 – 7.5 kwa hekta moja au umi kwa hekari.
MAPENDEKEZO YA MBEGU ZA KUPANDA
Kuna mbegu nyingi za kisasa zilizoko kwenye soko mfano wa
SIDCO ,PANNAR, CHOTARA, kutoka KENYA n.k Ni vyema
kufuata ushauriwa wataalamu wa kilimo
Idadi ya mimea katika eneo ni muhimu kwani ikazidi
- Mazao hupungua.
- Mmea huangushwa na upepo
- Mabua mengi hayazai.
Idadi ya mimea nayo ikipungua kwenya eneo husababishwa mavuno kupungua jambo la kufanya ni kupanda mbegu katika nafasi sahihi zilizoshauriwa na wataalamu.
KIASI CHA KUPANDA
- Mbegu za mahindi huhifadhiwa kwa dawa kali(sumu
- Kiasi cha kilo 20(ishirini) za mbegu kinatosha kupanda hekari moja., (Hii hutegemea na aina ya mbegu)
Nafasi za kupanda.
75cm x 30cm
75cm x 60cm
90cm x 25cm
90cm x 50cm
KANUNI YA TANO; KUTUMIA MBOLEA
Mahindi hustawi na kuzaa vizuri iwapo yatapatiwambolea pamoja na matunzo mengine ya kilimo bora. Ukipanda mbegu bora bila kutumia mbolea ni kazi bure.
- Mbolea za asili mfano; samadi,mboji na majani mabichi,mbolea hizi hua na virutubisho vya kutosh ambavyo havijulikani vipo kwa kipimo kiasi gani
- Mbolea za viwandani, hizi hua na virutubisho vya kutosha na vipimo hujulikana, hii inasaidia kujua ni kiasi gani kitumike kwa kipindi gani.
ULIMAJI WA MPUNGA
KILIMO CHA KISASA CHA MPUNGA
Utangulizi
Mpunga ni zao la pili la chakula kwa umuhimu linalolimwa sehemu nyingi nchini Tanzania. Umuhimu wa zao hili umeongezeka kuanzia muongo uliopita kutokana na jamii za mijini na vijijini kupendelea zaidi kula wali na kupunguza ulaji wa vyakula vingine na kulifanya zao hili kuwa la chakula na biashara.
Mvua ni chanzo kikuu cha maji kwenye kilimo cha mpunga. Viwango vya mahitaji ya maji katika kukua kwa mpunga hutofautiana miongoni mwa aina za mpunga. Ni kwa jinsi hii mpunga hupandwa katika mazingira mbalimbali kutegemea na mahitaji yake ya maji. Zipo aina tatu kuu za mazingira yanayolimwa mpunga kulingana na upatikanaji wa maji na hali ya mwinuko wa nchi. Mazingira haya ni kilimo cha mpunga wa mabondeni kinachotegemea mvua (72%), kilimo cha mpunga wa kwenye miinuko (20%) na kilimo cha mpunga cha umwagiliaji (8%).
Kiasi cha mpunga kinachozalishwa nchini kimekuwa kikiongezeka mwaka hadi mwaka kutoka tani 41,000 mwaka 1970 hadi tani 811,500 mwaka 1998. Ongezeko hili limetokana na kuongezeka kwa eneo linalolimwa mpunga na kwa kiasi kutokana na kuongezeka kwa miradi midogo ya umwagiliaji pamoja na matumizi ya tekinolojia bora za kilimo.
Maeneo yanayolima mpunga kwa wingi Tanzania: ni Morogoro maeneo ya bonde la kilombero/Ifakara, Dakawa, Malolo; Mbeya: Kyela, Mbarali; Shinyanga: Kahama; Mwanza, Bonde la Ruvu mkoani Pwani. Na maeneo mengine mengi
Shamba la mpunga |
pH ya udongo (Soil pH)
pH ni kipimo kinachoonyesha kiwango cha tindikali au nyongo katika udongo. Udongo waweza kuwa tindikali (ph ndogo kuliko 7), nyongo (ph kubwa kuliko 7), au katikati (neutral) - ph ya 7. Tindikali au nyongo ya udongo hupimwa kwa kutumia pH mita. Mazao mengi hustawi zaidi katika udongo wenye hali ya tindikali ya wastani (kipimo cha pH 5.5 hadi 7.0). Mpunga hustawi kwenye udongo wa mfinyanzi wenye tindikali ya wastani na virutubisho vya kutosha.
Kuandaa Shamba, Kupanda na Kupalilia
Kuandaa shamba, kusafisha, kulima/kutifua
Ni vyema mashamba yaandaliwe mapema kabla ya msimu wa kupanda haujaanza ili kumpa mkulima fursa ya kupanda kwa wakati unaotakiwa. Kuna njia mbalimbali zinazotumika kuandaa mashamba. Kati ya njia hizi ni pamoja na kufyeka, kung’oa visiki na kulima. Shamba linaweza kulimwa kwa kutumia:
- Jembe la mkono - wengi wanatumia
- Jembe la kukokotwa na wanyama kama ng’ombe
- Power tillers
- Matrekta
Baaada ya kulima, shamba linawekwa maji ili liloane vizuri na kisha udongo unachanganywa vizuri na maji ili kutengeneza tope. Hii ni kuchavanga (puddling). Hii inarahisisha:
- Kupandikiza miche
- Kuhifadhi maji
Mbegu Bora za Mpunga
Matumizi ya mbegu bora ni muhimu katika upatikanaji wa mavuno mengi na bora. Kuna makundi mawili makuu ya mbegu ambayo ni:
Mbegu za asili za mpunga: Ni zile ambazo zimetumika miaka mingi katika historia ya kilimo. Kuna aina nyingi za mipunga ya asili inayolimwa sehemu mbalimbali hapa nchini kama Supa, Kahogo, Kula na Bwana, Shingo ya mwali, n.k. Wakulima wanazipenda mbegu hizi kutokana na kuwa na sifa kama vile ladha nzuri, uvumilivu wa matatizo mbalimbali ya kimazingira na kwa sababu ya uwezo wa mbegu hizi kustahimili katika hali mbaya ya hewa na hazihitaji uangalizi wa hali ya juu.
Sifa hizi ni matokeo ya mbegu hizi kumudu mazingira na uchaguzi wa mbegu uliofanywa na wakulima kwa miaka mingi. Hata hivyo, nyingi ya mbegu hizi zina uwezo mdogo wa kuzaa, zinachelewa kukomaa, ni ndefu na rahisi kuanguka.
Mbegu zilizoboreshwa: Hizi ni zile zilizoboreshwa kutokana na mbegu za asili. Mfano wa mbegu zilizoboreshwa ni kama vile Katrin, IR54, na IR64. Zinazaa sana hasa kwa kilimo cha umwagiliaji. Hata hivyo, hazikidhi ladha ya walaji na ukobolekaji wake si mzuri na baadhi hazistahimili kwenye mazingira mengi ya kawaida. Hii imezifanya mbegu hizi kukubalika na wakulima kwa kiwango kidogo sana.
Mbegu bora nyingine zilizozalishwa kutoka utafiti na kuonekana kupendwa kwa ajili ya mavuno mengi na ladha nzuri kama TXD88 na TXD85. Hivi karibuni imetolewa mbegu nyingine iitwayo TXD306 (SARO5), mbegu hii hupendwa na wakulima, wafanyabiashara na walaji kutokana na sifa yake ya mavuno mengi, punje ndefu kiasi na nzito, ladha nzuri na yenye kunukia pindi ipikwapo na kuliwa.
Mbolea za kupandia mpunga
Kabla ya kuweka mbolea hakakisha kuwa majaruba yanatengenezwa ili kuhakikisha maji hayaingii na kutoka kiholela. Mbolea ya kupandia huwekwa kwa kusia katika jaruba kabla ya kuchavanga. Kuchavanga husaidia kuchanganya udongo na mbolea na pia kutengeneza eneo zuri la kupandikiza miche. Baadaye miche hupandikizwa.
Viwango vya mbolea za kupandia mpunga
Kiwango cha mbolea za kupandia kilichopendekezwa ni kilo 20 phosphate (P) kwa hektari ambayo ni sawasawa na kiasi mifuko mitatu kwa hekta ya DAP (= mfuko mmoja kwa ekari), au mifuko miwili kwa hekta ya Minjingu Phosphate (= mfuko mmoja na nusu kwa ekari) au mifuko minne na nusu kwa hekta ya Minjingu Mazao (= mifuko miwili kwa ekari).
Jinsi ya kupanda mpunga Kitaalam
Kuna njia mbili kuu zinazotumika kupanda mpunga shambani. Njia hizo ni ile ya kupanda mbegu moja kwa moja shambani na ile ya kupandikiza miche.
- Kupanda mbegu moja kwa moja
Njia hii hutumika kwa kupanda mbegu moja kwa moja kwenye shamba lililotayarishwa vizuri. Njia ya kawaida waitumiayo wakulima ni ile ya kumwaga na kufukia mbegu (broadcasting). Njia zingine ni zile za kupanda mbegu kwenye mashimo yaliyo kwenye mstari na kwa kuzingatia nafasi maalum au mbegu hupandwa kwenye mashimo bila kufuata mstari na bila kuzingatia nafasi iliyopendekezwa (dibbling). Vile vile mbegu hupandwa kwa kunyunyizwa kwenye vifereji vyenye vina vifupi na kufukiwa pasipo kuwa na nafasi kati maalum kati ya punje na punje (seed drilling)
- Kupandikiza miche
Njia hii hutumika kwa kupanda mbegu kwanza kwenye kitalu kabla ya kuzihamishia shambani. Mara nyingi mbegu zetu hutumia wiki tatu hadi nne baada ya kuota kwenye kitalu na kufikia umri wa kupandikizwa shambani. Katika shamba la mpunga miche hupandikizwa shambani kwenye mstari na kwa nafasi maalum au kupandikizwa holela bila kuzingatia nafasi maalum za kupanda.
Inashauriwa kupandikiza miche katika kina cha sentimeta 2 hadi 3. Ukipanda kina kirefu machipukizi huchelewa kujitokeza. Baada ya kupandikiza miche, machipukizi hujitokeza baada ya siku 5 hadi 10.
Kupandikiza miche ya mpunga |
Nafasi ya kupanda mpunga
Nafasi ya kupanda mpunga mbegu bora ni sm 15 kwa sm 15 au sm 20 kwa sm 20. Kwenye mpangilio wa mistari miwili miwili (double rows), nafasi kati ya mistari miwili ni sm 10, nafasi kati ya mmea na mmea katika kila mstari ni sm 20, na nafasi kati ya mistari miwili na mistari miwili mingine (double rows) ni sm 40. Mbegu za asili zipandwe kwa nafasi ya sm 20 kwa sm 20 au sm 25 kwa sm 25 au sm 30 kwa sm 30.
Kupanda kwa nafasi ni kati ya njia bora za kilimo inayomwezesha mkulima kupata mazao bora. Hivyo ni muhimu sana kuzingatia kupanda kwa mistari na kufuata nafasi zinazoshauriwa na wataalamu wa kilimo.
Muda wa kupanda
Muda wa kupanda unatofautiana kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na majira ya mvua. Kwa mfano katika wilaya ya Morogoro tarehe za kupanda ni kuanzia desemba hadi januari kwa mpunga wa muda mrefu. Kwa mpunga wa muda wa kati na muda mfupi, tarehe ya kupanda ni februari hadi machi.
Kupalilia Mpunga
Ni muhimu shamba lipaliliwe ili kuondoa magugu. Magugu ni mimea hivyo hushindana na mimea iliyopandwa na mkulima kwa kunyonya virutubisho ardhini. Magugu yanaweza pia kuhifadhi wadudu na magonjwa yanayoweza kushambulia mimea iliyopandwa na hivyo kupunguza mavuno.
Katika kilimo cha mpunga, ni muhimu shamba lipaliliwe siku 14 hadi 21 baada ya mimea kuota kufuatana na hali ya shamba wakati wa kupanda. Ni vizuri katika kilimo cha mpunga, shamba lipaliliwe mara mbili, kutegemeana na hali ya magugu katika shamba. Unaweza kupalilia kwa kung’olea kwa mkono, kwa mashine au kwa kutumua viua magugu (herbicides) kama vile 2, 4-D (Two Four D).
Utafiti unaonyesha kwamba, shamba la mpunga ambalo halijapaliliwa linaweza kupunguza mavuno kwa asilimia 60 hadi 100 ya mavuno yanayotarajiwa. Hata kama mkulima atatumia mbegu bora, aina na kiasi cha mbolea zinazoshauriwa, kupanda kwa mstari pamoja na mbinu nyingine bora zinazoshauriwa, bila kupalilia hali hii itaathiri mavuno yake.
Mbolea za kukuzia mpunga
Ni mbolea zinazotumika baada ya mimea kuota kwa lengo la kuikuza mimea ili itoe mavuno bora. Mara nyingi mbolea hizi zinatoa kirutubisho cha naitrojeni.
Kiwango kinachopendekezwa ni kilo 60 naitrogeni kwa hektari, ambacho ni sawasawa na kiasi cha mifuko miwili ya UREA au Minne na Nusu Ya CAN au Mitatu ya SA. Mbolea inayotumika mara kwa mara ni Urea. Hata hivyo mbolea zingine kama SA inaweza kutumika kama kuna mahitaji ya salfa. CAN inaweza kutumika kama kuna mahitaji maalum ya nitrate na ammonium. Kwenye mpunga, mbolea ya kukuzia inawekwa wiki mbili baada ya kupandikiza miche na irudie tena baada ya wiki nne.
Kuweka mbolea: Mbolea ya kukuzia hutiwa kwa kusia wiki mbili baada ya kupandikiza, na kurudia mwezi mmoja baadaye. Ni vyema kuweka mbolea za kukuzia mara mbili ya kiasi kinachopendekezwa.
Shamba la mpunga uliopandwa kwa mistari |
Kudhibiti Magonjwa na Wadudu Wanaoshambulia Mpunga
Magonjwa Yanayoshambulia Mpunga
Magonjwa ya mpunga yamegawanyika katika makundi matatu kulingana na vimelea visababishi ambavyo ni fungasi, virusi na bakteria.
i) Rice blast (Ukungu)
Unaosababishwa na Pyricularia oryzae.
Dawa/Kudhibiti: Mbegu bora inayostahimili ugonjwa, kupanda mapema, kung’oa mimea iliyoathirika ama kunyunyiza dawa za kuua ‘vectors’ kama vile inzi weupe (white flies).
ii) Brown leaf spot
Unaosababishwa na Helminthosporium spp.
Dawa/Kudhibiti: Panda mbegu kwa udongo unaofaa, weka mbolea ya kuzuia au tibu mbegu na dawa.
iii) Sheath rot
Unaosababishwa na Acrocylindrium oryzae.
Dawa/Kudhibiti: Kwa sasa hakuna njia ya kuzuia
iv) Rice Yellow Mottle Virus (RYMV) - Kimnyanga
Hivi karibuni ugonjwa wa kimyanga umetajwa kama ugonjwa hatari sana kwa mpunga hapa Tanzania.
Dawa/Kudhibiti: Panda mbegu zilizoboreshwa, zinazostahimili magonjwa au ng’oa mimea iliyoathirika.
Magonjwa yasababishwayo na bakteria nayo wametajwa kuwa na madhara makubwa kwa uzalishaji wa mpunga hapa nchini. Bakteria hawa wanajumuisha Acidovorax avenae subsp. Avenae asababishae ugonjwa wa bacterial stripe, Pantoea aglomerans, asababishae ugonjwa wa palea browning na Xanthomonas oryzae p.v. oryzae.
Wadudu wanaoshambulia mpunga
Kuna aina nyingi sana za wadudu wanaoathiri mpunga katika hatua mbalimbali za ukuaji wa mpunga. Wanapokithiri na wasipodhibitiwa hupunguza kiasi cha mavuno shambani.
i) White flies (Funza weupe)
Dawa/Kudhibiti: Nyunyiza dawa ya Thiodan, Endosulfan (Thionex), Fipronil (k.m. Regent 3G), Fenthion (k.m. Lebaycid)
ii) Rice stalk borer waharibifu
Kudhibiti: Nyunyiza dawa ya Thiodan, Endosulfan (Thionex), Fipronil (k.m. Regent 3G), Fenthion (k.m. Lebaycid) Ili mkulima aweze kupata mazao mengi na bora inashauriwa kutumia dawa za kuzuia magonjwa na wadudu wanaoshambulia mimea na njia zinginezo.
Kuvuna, Kukausha, Kusafisha na Kuhifadhi
Kuvuna: Mpunga uko tayari kuvuna wakati asilimia themanini (80%) ya rangi ya mpunga kwenye masuke imebadilika na kuwa dhahabu. Mpunga unavunwa kwa kukata bua pamoja na suke lake.
Uvunaji wa mpunga |
Kukausha: Rundika pahali pakavu k.m. kwenye tuta la jaruba halafu pigapiga (thresh) ili kutenganisha masuke na mpunga. Kama mpunga hayajakauka vizuri hukaushwa zaidi juani kwa siku 3-4 ili kupunguza unyevunyevu kufikia kiwango kinachofaa kwa kuhifadhi (14%). Ni muhimu mpunga ukauke vizuri ili usioze ukiwekwa ghalani.
Kusafisha: Mpunga uliyokauka vizuri hupepetwa na vilevile mapepe huondolewa.
Kuhifadhi: Mpunga safi huwekwa kwenye gunia na magunia kupangwa vizuri ghalani juu ya mbao yasiguse sakafu.
Acha comment yako hapa chini ili ku-share mawazo na wakulima wenzetu.
YOU MIGHT ALSO LIKE
-
MUONGOZO WA KILIMO BORA CHA MUHOGO
JULY 03, 2017 -
JE UNAMFAHAMU MDUDU HUYU HATARI KWA MAHARAGE?
MAY 29, 2017 -
KILIMO BORA CHA MAHARAGE
MAY 22, 2017
POST A COMMENT
OUR SPONSORS
POPULAR POSTS
RECENT POSTS
-
Jumatatu iliyopita nilikuandikia...
-
Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya...
-
Ndugu mkulima, ili ufanye kilimo bora...
-
Mkulima ni mfanyabiashara, na...
-
Funza wa vitumba ni nondo, na ni mdudu...
RANDOM POSTS
-
28.05.2016 - 0 Comments
-
09.06.2016 - 3 Comments
-
17.06.2016 - 0 Comments
-
28.01.2017 - 5 Comments
-
05.07.2016 - 0 Comments
AUTHORS
FOLLOW ME ON GOOGLE +
CATEGORIES
FURSA NA AJIRA (8)GOOD AGRIC. PRACTICES (1)KILIMO BIASHARA (1)KILIMO BORA (29)KILIMO CHA MAHINDI (4)KILIMO CHA MATANGO (1)KILIMO CHA UYOGA (2)MAZAO YA VIUNGO (6)MBEGU BORA (1)MIGOMBA (4)NAFASI ZA KAZI (28)NYANYA (3)UFUGAJI (5)UFUGAJI WA KUKU (5)VANILA (2)VIAZI VITAMU (1)VITUNGUU (2)WADUDU NA MAGONJWA YA MIMEA (4)
CREATED BY SORATEMPLATES & MYBLOGGERTHEMES
1 comment: